YANGA NA KAZE MAMBO MAGUMU
HABARI ZA MICHEZO : KOCHA Msaidizi wa Yanga, Mrundi Cedric Kaze amekataa kusaini mkataba mpya wa timu hiyo, akitoa masharti magumu kwa uongozi ulioanza mazungumzo ambao ulitarajiwa kukutana jana usiku kuacha mchakato wa kumpata kocha mkuu mpya. Mkataba wa Nabi na Kaze ulimalizika Jumatatu hii mara baada ya mchezo wa Fainali ya Kombe la FA kumalizika kwa Yanga kutwaa taji hilo kwa kuwafunga Azam FC bao 1-0 lililofungwa na Kennedy Musonda uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Mmoja wa Mabosi wa Kamati ya Utendaji ya Yanga ameliambia Championi Ijumaa kuwa, jana mazungumzo yalishindwa kufikia muafaka mzuri kati ya uongozi na Kaze ambaye ameomba afanyiwe maboresho katika mkataba wake mpya. Bosi huyo alisema kuwa kikubwa ameutaka uongozi wa timu hiyo, kuongeza ofa ya kuongeza mkataba na mshahara ambayo ni siri aendelee kubakia hapo Jangwani. Aliongeza kwa kutoa sharti la kuchukua dau hilo la kumbakisha na mshahara huo, lakini awe kocha mkuu na sio msaidizi kama ilivyokuwa awali. “Mar