Posts

Showing posts from April 27, 2017

DIWANI APELEKWA POLISI KISA MWENGE

Image
         Diwani wa katia ya kitwiru kwa tiketi ya chadema manispaa ya iringa Baraka Kimata ameshikiliwa na polisi kwa muda baada ya kutoa maneno yaliyotafsiliwa kuwa ni ya kashifa kwa mbio za mwenge . Kimata ambaye pia ni katibu mwenezi wa chama cha Chadema Manispaa aliitwa jukwaani kuongea kwa niaba ya chama chake cha Chadema baada ya katibu wa CCM kuongea . Kimata pamoja na mambo mengine aliyoongea alimalizia kwa kusema kuwa kama CHADEMA ikipewa ridhaa ya kuongoza nchi basi wataupumzisha mwenge wa Taifa . Baada ya hapo wasemaji wote waliofuata akiwemo mkuu wa wilaya ya Iringa na mkimbiza mwenge walimshambulia Kimata na chama chake kwa msimamo huo wa kupinga mbio za mwenge wa Taifa . Baadaye Kimata alikamatwa na kupelekw kituo kikuu cha polisi kuhojiwa na kuachiliwa . Habari kutoka kwa watu wake wa katibu zinasema kuwa Kimata anatakiwa kuandika barua ya kuomba msamaha .

ALIKIBA APATA MCHONGO LONDON BAAD YA KUTOKA MAREKANI

Image
        Msanii wa bongo Fleva Alikiba ambaye anafanya vizuri na wimbo wake wa aje , amepata nafasi ya kushiriki katika tamasha kubwa la mitindo huko London .  Kupitia ukurasa wake wa Instagram Alikiba amewajuz mashabiki wake kwa kupost ujumbe unaoonyesha na kuwajuza mashabiki wake kuwa kapata nafasi ya kutumbuiza katika tamasha hilo linalokwenda na kudfahamika kama One Afrika Premium Fashion litakalofanyika tarehe 12 mwezi wa 5 jijini London akiwa na wasanii wengine kama Victoria Kiman ,  Fleviour, Bank W,  Tiwa Savage na wengine.  Shindano la One Afrca Fashion at the heart of London.   Alikiba bado yupo nchini Marekani ambapo anaendelea na tour yake akiwa pamoja na ndugu yake Abdukiba .

MVUA YAUA WANAFUNZI WAWILI NA KUJERUHI ANNE MKOANI SIMIYU

Image
       Wanafunzi wawili wa shule ya msingi Kasoli wakiwa ni ndugu wa familia moja wamefariki dunia huku wengine wanne wakiwa wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta wa kanisa la ACT la kasoli wakiwa wamejikinga na mvua iliyokuwa ikinyesha na kuambatana na upepo mkali .    Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu Bonaventure Mshongi amesema ajali hiyo ilitokea tarehe 24 aprili katika kijiji na katia ya Kasoli tarafa ya Mhango wilaya ya bariadi mkoani Simiyu ambapo baadhi ya majeruhi wamelazwa katika hospital teule ya mkoa wa Simiyu na hali zao zinaendelea vizuri.