MATOKEO YA LIGI KUU VPL TANZANIA BARA LEO TAR: 10 April.
Michezo ya leo ya ligi kuu Vodacom ilikuwa miwili tu ambayo ni : Mbao v/s Simba (Ccm kirumba -Mwanza ) Mtibwa Sugar v/s Azam F c (Kaitaba-Morogoro) Matokeo ya michezo hiyo ni . Mbao 2-3 Simba , huu ni mchezo ambao Mbao fc walikuwa wanaongoza kwa goli mbili mpka dk ya 83 ambapo mshambuliaji Blagnon aliipatia simba goli la kwa dk 83 kwa mpira uliopigwa na kuuparaza kwa kichwa . Lakini pia dk ya 90 +2 Blagnon aliipatia Simba goli la pili baada ya golikipa kujichanganya na mpitra uliopigwa juu na kudunda miguuni mwake na goli la tatu la simba lilifungwa na Mzamiru Yasini dk ya 90 +7 baada ya kutulia na kupiga shutu lililomzidi golikipa wa mbao fc . Mchezo ulikuwa mkali sana hasa baada ya kipindi kwa kwanza ambapo wachezaji wa mbao walionekana kuupania sn mchezo ambapo walijipatia magoli yao mawili kipindi cha kwanza kupitia kwa washambuliaji wao ambao ni Sangija dk 18 aliipatia mbao fc goli la kwanza kabla ya Evarsti dk ya 32 kuipatia mbao fc goli la pili .