Posts

Showing posts from March 22, 2017

WAZIRI NAPE NNAUYE APIGWA CHINI , MWAKYEMBE ACHUKUA NAFASI .

Image
   Baraza la mwaziri la Tanzania lafanyiwa mabadiliko kidogo hii ni baada ya waziri Wa Sanaa michezo na utamaduni Nappe Nnauye kuondolewa kwenye cheo chake .  Raisi Wa jamhuri ya muungano Wa Tanzania mh Dk. John Pombe Magufuli leo tarehe 23/3/2017 amefanya mabadiliko madogo katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo Rais amemteua Prf. Palamaganda John Aidan Mwaluko Kabudi kuwa waziri Wa katiba na sheria huku akimteu Dkt. Harson Mwakyembe kuwa waziri Wa sanaa , michezo na utamaduni  . Uteuzi juu unaanza Mara moja na kesho tarehe 24/3/2017 mchana wataapishwa ikulu jijini Dar es salaam .                                      Gerson Msigwa                        Mkurugenzi Wa mawasiliano                                 Ya Rais IKULU .                               Dar es salaam

VYOMBO VYA HABARI VYAGOMA KUSHIRIKIANA NA MKUU WA MKOA WA DSM PAUL MAKONDA.

   Baada ya mkuu Wa mkoa Wa Dar es Salaam kuvamia Clouds media na kuwalazimisha watangazaji Wa kipindi cha Shilawadu kurusha kipindi kurusha kipindi kinachomhusu Mch. Gwajima kikiwa hakijamaliziwa maandalizi kinyume na taaluma ya habari Jana machi 22, 2017 Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) kimefanya kikao cha maamuzi juu ya suala hilo kuwa hawatotoa ushirikiano wowote na mkuu Wa mkoa huyo ambaye amekuwa akitumia vyombo vya habari katika mikutano yake na shughuli zake za kutimiza majukumu yake. Pia jukwaa hilo limesema kuwa Kwa mwandishi atakaye husika au kutoa ushirikiano na mkuu Wa mkoa huyo , kitendo chochote kitakachomkuta jukwaa hilo halitahusika Kwa namna yoyote ile .

SOMA RIPOTI YA KAMATI YA UCHUNGUZI KUHUSU MKUU WA MKOA WA DSM PAUL MAKONDA KUVAMIA CLOUDS MEDIA.

Image
   Baada ya tukio La mkuu Wa mkoa Wa DSM, PAUL MAKONDA kusemekana kuwa alivamia kituo cha matangazo na Televisheni cha Clouds . Waziri Wa Sanaa michezo na utamaduni Mh. Nape Nnawiye aliamua kuunda kamati ya kuchunguza tuhuma hizo na hii ndyo ripoti ya UCHUNGUZI Wa kati hiyo . Waziri Nape Nnawye amepokea ripoti ya kamati ya uchunguzi aliyoiunda . Balile: Tulifanya mahojiano na wafanya kazi 14 Wa kituo cha             clouds . Balile:Tulifanya juhudi za kumtafuta mkuu Wa mkoa Paul             Makonda Kwa kumpigia simh lakini hakupokea . Balile:Hata tulipofika katika ofisi zake aliondoka kupitia            Mlango Wa nyuma. Balile:baada ya kushimdwa kuonana naye tukajiridhisha                    kuwa amechagua mwenyewe kutotumia fulsa ya                        kuhojiwa. Balile:katiak a uchunguzi wetu tumejirishisha kuwa mkuu            Wa mkoa Wa dar es salaam aliamua kuvamia kituo           Cha clouds akiwa anaendesha gari mwenyewe. Balile:kamati imejiridhisha kuwa RC na as