Posts

Showing posts from April 26, 2017

MBAO WASEMA YANGA HATOKI MWANZA KOMBE LA SHIRIKISHO NUSU FAINALI

Image
              Katika kuelekea hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho (FA) ,  timu ya mbao Fc imeanza kujitapa kuwa wapo tayari kuwapokonya ubingwa wapinzani wao yanga siku ya jumapili huku wakisisitiza kuwa wapo tayari .

NAPE NNAUYE AFUNGUKA KUHUSU CCM YA MAGUFULI

Image
                     Ikiwa leo Tanzania imetimiza miaka 53 tangu kuungana kwa nchi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar zjlizoungana mwana 1964 . Mbunge wa jimbo la Mtama Mh. Nape Nnauye  amefunguka na kusema kuwa CCM ndiyo waasisj wa muungano huo.     Nape amesema licha ya kuwepo kwa mapungufu ya hapa na pale lakini bado kitabakia kuwa ndicho chama bora cha mfano barani Afrika . Nape ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Twiter .    "CCM ndicho chama bora cha mfano barani Afrika ,  Ni imara na kina historian ndefu nzuri iliyotukuka sana . Ndiyo waasisi wa muungano wetu , tuudumishe alisisituza Nape.

HALIMA MDEE AOMBA MSAMAHA KWA KUMTUKANA SPIKA WA BUNGE.

Image
               Mbunge wa jimbo la kawe kwa tiketi ya Chadema Mh.  Halima Mdee jana amefunguka na kuomba msamaha bungeni kufuatia kutoa lugha isiyo na sitaha bungeni wakati wa uchaguzi wa wabunge wa bunge la Afrika mashariki uliofanyika tarehe 4 , april 2017 .   Halima Mdee wakati akiomba radhi amesema kuwa wakati tukio hilo linatokea siku hiyo bungeni kulikuwa na matukio yaliyokuwa yakiendelea bungeni ambayo yalimpelekea kutoa lugha isiyo sawa kitamaduni za bunge ,  ambayo ilimgusa spika wa bunge na Naibu waziri wa wizara ya afya ,  maendeleo ya jamii , jinsia,  wazee na watoto Dkt.  Hamisi Kigwangala .

MWANJALE AANZA MAZOEZI CHINI YA UANGALIZI WA DAKTARI.

Image
        Beki wa kikosi cha Simba Method Mwanjale ameanza mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa Daktari. Mwanjale aliumia na amekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi miwili sasa .  Sasa ameanza mazoezi mepesi na Mratibu wa Simba Abasi Ally "Gazza" amesema kila kitu kinafanyika chini ya uangalizi .  "Daktari ndiye anasimamia kila kitu , hivyo anajua nini anatakiwa kufanya ingawa ameanza mazoezi mepesi chini yake " alisema Gazza   Mwanjale yuko Morogoro na kikosi cha simba ambacho kimeweka kambi huko kujiandaa na mechi dhidi ya Azam kwa ajili ya nusu Fainali ya kombe la Shirikisho .    Simba imekuwa ikiyumba katika safu yake ya ulinzj kutokana na kumkosa Mwanjale raia wa Zimbabwe ambaye amkuqa ni tegemeo kubwa katika kikosi hicho .

YANGA YAZDI KUPATA MAMILIONI.

Image
             Ikiwa ni siku moja baada ya uongozi wa yanga kuanza harambee ya ukusanyaji wa fedha kwaajili ya kuisaidi klabu hiyo, tayari klabu hiyo imeanza kupokea fedha mbalimbali kutoka kwa wadau na mashabiki wa soka mbalimbali.   Juzi uongozi wa yanga ulizindua harambee kwa ajili ya watu mbalimbali kuichangia fdha timu hiyo ili iweze kuendelea na shughuli zake za kimaendeleo zoezi ambalo limeanza kwa kishindo kikubwa .   Katibu mkuu wa klabu Charles Boniface Mkwasa" amesema fedha hizo zitakuwa ni kwaajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo kuwalipa mishahara wachezaji wake ambao wanadai mwezi uliopita na ujao .   Mkwasa amesema anashukuru sana kwakuwa zoezi la uchangishaji limepokelewa vizuri sana na wanachama kwani wenye mapenzi wameanza kujitoa kwa hali na mali . "Klabu inathamini mtu kwa kiwango chochote anachotoa , pia tunatanguliza shukrani za dhati na kutambua umuhimu wa kila mmoja katika mchakato huu." alisema Mkwasa.  Alisema pia uongozi utakuwa un