Posts

Showing posts from July 3, 2023

SIMBA SC HAPA NDIPO KAMBI YA PRE SEASON ITAPOKUWA .

Image
HABARI ZA MICHEZO ... 🚨 || RASMI, IMETHIBITISHWA: ☑️ Simba SC🇹🇿 kuweka kambi ya Pre-season nchini Uturuki 🇹🇷 Klabu ya Simba SC imetangaza kuwa itaweka kambi ya Wiki tatu Nchini Uturuki 🇹🇷 kwaajili ya kujiandaa na Msimu Mpya wa Mashindano wa 2023/24. Wachezaji wote waliosajiliwa na Simba na wale wa zamani watakuwa sehemu ya Kambi hiyo huku wakitarajia kucheza Michezo mitatu dhidi ya timu za Uturuki 🇹🇷 kabla ya kurejea Nchini Mwishoni mwa mwezi huu. #sam_misangletz  Whatsap  : +255629552663 

MSHAHARA WA MESSI INTER MIAMI HUU HAPA SASA .

Image
HABARI ZA MICHEZO. Mmiliki mwenza wa klabu ya Inter Miami, Jorge Mas amethibitisha kuwa mshambuliaji mpya klabuni hapo Lionel Messi atapokea mshahara kati ya euro milioni 45-55 kila mwaka . "Mazungumzo yalidumu kwa miaka mitatu, ikijumuisha mwaka mmoja na nusu wa mazungumzo makali sana" MESSI PIA ATAPOKEA:  ▪️Asilimia kadhaa ya mauzo ya jezi za klabu hiyo.  ▪️Sehemu kwenye usajili wa Apple TV ya MLS ▪️Hisa za Franchise baada ya kustaafu. NB: Mshahara huo wa Messi kwa mwaka ni kati ya Tsh bilioni 119 mpaka Tsh bilioni 145 kwa mwaka. ✍️ Hata hivyo mshahara huo wa Messi ni kiduchu sana ukilinganishwa na mshahara wa hasimu wake wa muda mrefu, Cristiano Ronaldo anayelipwa Tsh bilioni 530 kwa mwaka huko Al Nassr FC ya Saudi Arabia. Via #kitengeMaulid #sam_misangletz 

NEWCASTLE UNITED WAMWAGA PESA KUFURU BIL. 183

Image
HABARI ZA MICHEZO #MICHEZO Klabu ya Newcastle United ya Ligi Kuu England EPL imekamalisha usajili wa kiungo Sandro Tonali kutoka AC Milan ya Italia kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 60 zaidi ya Bilioni 183 na milioni 999 kwa pesa ya Tanzania. Tonali raia wa Italia ana umri wa miaka 23 amesaini mkataba wa miaka 5 kujiunga na Newcastle United. Tonali ameweka rekodi kuwa mchezaji ghali zaidi aliyenujuliwa na Newcastle akivunja rekodi ya Alexander Isak ambaye alijiunga na Newcastle kwa dau la Pauni milioni 55 akitokea Real Sociedad.  Huu ni usajili wa kwanza kwa Newcastle United kwenye dirisha hili kubwa la usajili kuelekea msimu ujao wa 2023-24. #NewcastleUnited #SandroTonali