Posts

Showing posts from March 29, 2017

MCHEZO WA YANGA NA AZAM PATACHIMBIKA .

Image
      Ligi kuu weekend hii inarejea tena kwa michezo kadhaa. Moja ya mechi kali ni YANGA na AZAM ,  je yanga watakubali kipigo tena kutoka kwa Azam ?  Au Azam watakubali kupigwa na Yanga ili kulipizia kipigo cha kombe la mapinduzi ?  Majibu utayapata kupitia hapa kama utakuwa mbali na runinga yako .

MECKY MEXIME : SIMBA LAZIMA TUWAFUNGE KAITABA.

Image
           Kocha mkuu wa timu ya Kagera Sugar Mecky Mexime amibuka na kusema kuwa wamejipanga kuhakikisha kuwa wanakatisha mbio za ubingwa kwa timu ya Simba S C , kwa kufanikiwa kuibuka na pint 3 katika mchezo wao utakaopigwa siku ya jumatatu pale kaitaba .        Kagera Sugar inatarajia kukutana na Simba april 3 katika uwanja wa kaitaba mjjni bukoba kwenye mchezo ambao unatarajiwa kuwa wa kiupinzani mkubwa kutokana na historia ya timu hizo zinapokutana .     Kagera Sugar ipo nafasi ya nne ya msimamo wa ligi ikiwa na point 42 nyuma ya Azam FC yenye point 44 , huku Simba ikiwa inaongoza ligi ikiwa na point 55 ikiwa imepania kuchukua ubingwa wa ligi kuu msimu huu baada ya kuukosa kwa muda mrefu .      Mexime amesema kuwa timu yake ipo vizuri na imejipanga vizuri kuelekea mchezo huo na kusema hawatakubali kupoteza point tatu zote kwa simba na badala yake anajipanga kuona wanakatisha mbio za ubingwa kwa Simba .                                     Imeandaliwa na            

SANCHEZ KUTUA CHELSEA YA England.

Image
          Kocha wa klabu ya chelsea Antonie Konte anampango wa kumsajili mchezaji wa Arsenal Alex Sanchez majira ya joto  kwa mujibu wa habari kutoka Guardian .            Muitaliano huyo ambaye kwa sasa anafanya mazungumzo ya mkataba mpya na klabu yake na amefanya mjadala kuhusu masuala ya usajili na klabu yake na hivyo kuwa mstari wa mbele katika kumhitaji mchezaji huyo raia wa Chile anayetaka kuondoka Emirates majira ya joto.         Alex amekerwa na maendeleo ya kikosi hicho cha Arsenal kisicho na maendeleo ya soka ,  pia klabu za PSG, JUVENTUS na INTER MILAN zinaonyesha nia yao ya kumhitaji star huyo .  Imeandaliwa na 👇👇👇👇      Misango Samweli. 

SOMA MAGAZETI YOTE YA LEO TAREHE 29 MACH 2017.

Image
        Nimekusogezea magazeti yote yaliyotoka leo March 27 mtanzania mwenzangu unaweza kujisomea hapa .