KIONGOZI WA FREEMASON ACHOMWA MOTO
Mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha freemason Afrika mashariki Sir. Chande umeteketezwa leo kijitonyama jijini Dar es Salaam , kupitia tukio lililodumu kwa takribani saa nzima . Mwili huo umeteketezwa kwa moto kupitia ibada iliyofanyika ndani ya nyumba maalumu inayofanyika kama sehemu ya mziko ya waumini wa dini ya Hindu . Sir. Chande alifariki siku tano zilizopita wakati akipata matibabu katika hspitali Nairobi nchini Kenya baada ya kuugua kwa muda mrefuugonjwa uliotokana na matatizo ya utumbo mdogo kusambaza sumu mwilini.