FAINALI YA FA , SIMBA NA MBAO KUPIGWA DODOMA
Baada ya kuwepo kwa story nyingi kuhusu uwanja utakao tumika katika fainali za michuano ya Kombe la Azam Federation sasa uwanja umetangazwa rasmi . Uwanja wa jamhuri mjini Dodoma ndiyo utakaotumika katika fainali za michuano hiyo kati ya Simba na Mbao siku ya mei 28 , 2017 Kwamjiibu wa kanuni Simba ndiyo wenyeji kwenye fainal hizo kwani ndyo walikuwa washindi wa kwanza kufuzu katika kuingia Fainali za michuano hiyo baada ya kuifunga Azm katika hatua ya nusu faunal huku Mbao wakiwafunga Yanga katika hatua ya nusu faunal katika uwanja wa ccm kirumba kwanza . Kabla ya uwanja huo kutajwa kuwa utatumika katika faunal hizo kulikuwa na maneno mengi sana kutoka kwa wadau wa soka katika mitandao ya kijamii ambapo wadau walikuwa wakijadili tweet ya rais wa TFF kwamba kutakuwa na draw kwaajili ya kutafuta uwanja wa fainali hiyo .