Posts

Showing posts from March 1, 2017

RAMADHANI KESSY AMEONYESHA UWEZO MKUBWA MCHEZO DHIDI YA RUVU SHOOTING

Image
   Hakika tuachane na ubishi na uzambiki km kweli unaujua mpira Wa miguu utakubaliana na mimi kuwa , mchezaji Wa YANGA  Ramadhani Kessy katika mchezo uliopita alionyesha nia yake ya kumshawishi kocha Lwandaminina kuendelea kumpatia nafasi katika kikosi cha kwanza baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo uliopita dhidi ya Ruvu Shooting ambapo Yanga waliibuka na ushindi Wa goli 2-0 .   Mchezaji huyo Wa zamani Wa wekundu Wa msimbazi amekuwa hapatiwi nafasi Mara Kwa Mara katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo huku akipatiwa nafasi Juma Abdul ambaye hata hvyo amekuwa hana kiwango kizuri toka atoke majeruhi kwani inasemekana alikuwa ameongezeka uzito   Ramadhani Kessy alicheza Kwa kiwango kikubwa sn kwn aliweza kupiga krosi nyingi sn , lkn pia aliweza kutoa pasi nyingi sn za mwisho sema wamaliziaji hawakuwa makini , Kessy aliweza kupiga mashoot golini na shuti moja liligonga mwamba wa juu Wa goli na kusababisha taflani kubwa Kwa wapinzani wake . Kwa kiwango alichoonyesha n

BARCELONA YAPIGA MTU 6-1 WAKATI REAL MADRID WAKITOA SARE 3-3

Image
         Timu ya Barcelona Jana imeibuka na ushindi Wa goli 6-1 dhidi ya Sporting Gijion na kiwafanya kufikisha point 57 katika msimamo Wa ligi kuu Spain .         Wakati Barcelona wakiibuka na ushindi huo timu ya Real Madrid wamebanwa mbavu na timu ya Las Palma's na kutoka sale ya goli 3-3 .  Baada ya michezo hiyo kumalizika timu ya Barcelona imeshika nafasi ya kwanza katika msimamo Wa ligi hiyo na kufuatiwa na Real Madrid ingawa Real Madrid anamchezo mmoja mkononi

MAMA SALIMA KIKWETE ATEULIWA KUWA MBUNGE

Image
       Mke Wa rais mstaafu , jakaya mrisho kikwete ameteuliwa leo kuwa mbunge Wa bunge la jamhuri ya muungano Wa Tanzania leo hii ikulu na Rais MAGUFULI . A Awali taarifa zilienea kuwa ameteuliwa kuwa mbunge Wa viti maalumu na baada ya muda marekebisho yalitolewa kuwa ni mbunge Wa bunge la jamhuri ya muungano Wa Tanzania na si mbunge Wa viti maalumu .

UJIO MPYA WA MC DARADA KAA TAYARI.

Image
Tazama msanii JACOB STEVEN ( JB)  alivyoamua kumwaga pesa Kwa mchezaji Wa simba aliyepelekea furaha Kwa mshabiki huyo Wa simba KICHUYA .

YANGA WASHINDA MECHI WAKIWA PUNGUFU TAIFA.

Mabingwa watetezi Wa ligi kuu Tanzania bara YANGA wameibuka washindi katika mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting walioshinda 2-0 na kufanya kuwa kayika nafasi ya pili na point 52 wakizidiwa na SIMBA  Kwa point 2 tu ambao wanapoint 54 mpk sasa ikiwa zimebaki mechi takribani saba ligi kuu kumalizika  Mabingwa hao wameibuka na ushindi huo baada ya SAIMON MSUVA kuipatia YANGA goli la kwanza Kwa njia ya mkwaju Wa penalt baada ya Chirwa kumbabatisha mchezaji Wa wapinzani mpira katika mkono , kabla ya mchezo kumalizika zikiwa zimebaki dk 4 mchezo kumalizika Emanuel aliipatia goli la pili timu yake na kupoteza matumaini ya wapinzani hao kusawazisha  Akizungumza baada ya mchezo Nahodha Wa timu ya YANGA amewashukuru wachezajj wenzake Kwa kujituma na kusema mchezo unaofuata dhidi ya mtibwa amesema kuwa utakuwa mchezo mgumu ila watajipanga kuhakikisha wanaibuka washindi .

LWANDAMINA : MECHI MOJA HAIWEZI KUTUNYIMA UBINGWA

Image
Kocha mkuu Wa mabingwa watetezi Wa ligi kuu Tanzania Bara LWANDAMINA amesema kuwa mashabiki Wa timu hiyo hawatakiwi kukata tamaa kutokana na kupoteza mchezo uliopita dhidi ya wekundu Wa msimbazi weekend iliyopita Kwa kipigo cha 2-1 . Akizungumzia mchezo Wa Wa leo dhidi ya RUVU SHOOTING kwenye uwanja Wa taifa amedai kuwa ushindi upo wamejipanga vizuri hivyo mashabiki hao wasikate tamaa YANGA itashuka uwanjani Leo ikiw na kikosi chenye mabadiliko ya wachezaji watano ambapo watakao anza nipamoja na HASSAN KESSY, MWASHUYA , BOSOU , KASEKE na KANAVARO .