HII NDIYO SABABU YA MAALIM SEIF KUTUMBULIWA CUF.
Baraza kuu la uongozi Taifa (CUF) leo ljmemvua Maalim Seif nafasi yake ya katibu mkuu wa chama hicho na nafasi yake kuchukuliwa na Bi. Magdalena Sakaya . Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo, mwenyekiti wa CUF anayetambulika na msajili wa vyama vya siasa Taifa Prf. Ibrahim Lipumba amesema baraza hilo limefikia uamzi huo kutokana na sababu mbalimbali ikiwa mojawapo ni kuwa Maalim Seif kutofika ofisini na kutohudhuria vikao vya chama vinavyotambuliwa na katiba ya chama hicho . "Miongoni mwa ajenda tulizojadili ni kuthibitisha wakurugenzi na manaibu wakurugenzi , kupitisha majina ya wagombea ubunge wa bunge la Afrika Mashariki , kujaza nafasi za wajumbe wa baraza kuu zilizokuwa wazi , kuunda bodi ya wadhamini , kuunda kamati ya maadili , taarifa ya kesi , fedha na taarifa ya hali ya hewa ya kisiasa . Pia Prf. Lipumba ametangaza nafasi ya majina matatu ya wagombea ubunge katika bunge la umuiya ya afrika mashariki kpitia majna yaliyopendekezwa na kikao cha