OMOG AFUNGUKIA USAJILI WA YANGA NAKUSEMA HAYA .
Kocha mkuu wa klabu ya Simba Joseph Omog amefungukana kuusifia usajili wa wapinzani wake kwa kusema kuwa uko vizuri hasa kwa kumtwaa mshambuliaji Ajibu ambaye yuko vizuri na atawasaidia katika msimu ujao wa ligi kuu ya VPL inayotarajiwa kuanza tarehe 26 August 2017 . "Yanga wamefanya usahili mzuri hasa kwa kumsajili mshambuliaji wetu Ibrahimu Ajibu ambaye aliuwa msaada mkubwa kwetu katika msimu uliopita na kutusaidia kutwaa kombe la FA la Azam Federation Cup , lakinj suala la nyota hao kama wtatamba pia katika msimu ujao nisuala la kusubiria kwani mchezaji anaweza kuwa mzuri katika msimu huj na ujao kiwango chake kikawa tofauti na awali hivyo tungoje msimu uanze ." Alisema Omog .