Posts

Showing posts from March 31, 2017

YANGA YAPATA MTIHANI KUELEKEA MCHEZO NA AZAM FC .

Image
       Kuelekea kwenye mchezo wa kesho jumamosi dhidi ya Azam FC ,  benchi la yanga lipo kwenye mtihani mzito juu ya kupanga kikosi chake kitakachokuwa na uhakika wa kupata ushindi .    Yanga haitakuwa na huduma ya mabeki wake Elvine Yondan,  Ramadhan Kessy ambao watajkosa mchezo huo kutokana na kuwa na kadi tatu za njano .   Pia yanga itamkosa mshambuliaji wake mrundi Hamis Tambwe ambaye anauguza majeraha , kocha wa timu hiyo Lwandamina alisema hayo kuwa hiyo ni changamoto kubwa kwa benchi lake lakini wanafanya kila linalowezekana ili kupata ushindi huo wa point tatu.      "Bado kuna wachezaji wengine ambao wanaweza kucheza na kuziba nafasi hizo , mambo kama hayo yanatokea kwenye timu huwezi ukawa na wachezaji wote wakawa vizuri bila majeraha kwenye mechi zote " lisema Lwandamina .         Lwandamina alisema kuwa habari nzuri kwao ni kurejea kwa mshambuliaji wao Donald Ngoma ambaye amekuwa na majeraha ambaye jana alitarajiwa kuanza mazoezi ya pamoja na wachezaji wenza

NAY WA MITEGO AKATAA KUUFANYIA WIMBO WA WAPO MAREKEBISHO.

Image
      Msanii wa kizazi kipya miondoko ya Hip Hop aliyeachia wimbo mpya hivi karibuni unaokwenda kwa jina la Wapo uliosababishwa kukamatwa kwake na kukaa selo kwa saa kadhaa na wimbo huo kupigwa stop na Basata kwa madai kwamba wimbo huo unaikashifu serikali  kabla ya Rais Dk .  John Pombe Magufuli kuamuru aachiwe na kumpongeza kwa utunzi wake huku akimwambia kuwa, aongeze na mambo mengine katika wimbo huo .       Msanii huyo ameibuka na kusema kuwa hawezi kufanya marekebisho na hapingani na mhe.  "Haikuwa kwa ubaya , hakuna cha kurekebisha kwenye wimbo wetu wa wapo ila aliyosema Mh. tutayafanyia kazi .  Huu ni wmbo wenu mashabiki wangu wote Tanzania na Duniani kote , WAPO ni wimbo ambao ujumbe umeanza kufika . Hakuna ata kay eba dili sha mtizamo wangu alisema .

SIRI YA DIAMOND KUFANIKIWA YAFICHUKA .

Image
       Nyota wa mziki w bongofleva nchini Nassib Abdul (DIAMIND PLUTNUM ) amefichua moja ya siri ya mafanikio yake makubwa nchini kuwa ni kuwasaidia watu wenye uhitaji.    Diamond ambaye anatajwa kuwa ndiye mwenye kipato kikubwa amesema kuwa anajisikia fahari kuona kuwa amekuwa kiwsidia watu wenye uhitaji na amekuwa akipata brka zaidi anapokuwa anawasaidi watu.     "Unajua watu wengi hawajui kuwa ukitoa unazidi kubarikiwa , hii kwangu imekuwa sehemu ya mafanikio sana , huwa najisikia mwenye bahati kubwa nikimsaidia mtu mwenye uhitaji kwani naamini lazima nitafanikiwa " alisema Daiamond.  Amesema amekuwa akikutana na changamoto nyingi ikiwemo watu wengi kuhitaji msaada kutoka kwake amesema kuwa amekuwa akilenga wale anaoamini wanahitaji msaada zaidi kutoka kwake Imeandikwa na      Misango Samweli  Whatsap                                             0625954293.

UHAKIKI WA VIGOGO WENYE VYETI FEKI .

Image
        Ikulu yamutwisha mzigo waziri.    Wakati uhakiki wa vyeti kwa wathmishi wa uma ukikamilika leo ,  ikulu imemtwisha mzigo waziri wa Nchi, Ofisi ya rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) ,  George SimbaChawene kuwa ndiye mhusika wa suala hilo .   Kwa mjibu wa tangazo lililotolewa march 20 mwaka huu na katibu mkuu Ofis ya Rais ,  Manejiment ya utumishi wa uma na utawala bora Dk.  Laurian Ndumbalo ,  uhakiki wa vyeti vya elimu na taaluma pamoja na namba za mitihani kwa watumishi wa umma ulioanza march 12 mwaka jana utakamilika rasmi leo.    Katika tangazo hilo Dk.  Ndumbalo amesema kuwa uhakiki huo haujalenga kumkomoa mtumishi wa umma bali kuhakikisha kuwa na watumishi wenye sifa zinazotakiwa kitaaluma na kitaalamu ili kutoa huduma zilizo bora na kwa weledi kwa wananchi.   "Serikali inasisitiza kuwa mtumishi wa umma atakayeshindwa kutumia muda uliotolewa ili kuwasilsha nakala za vyeti au namba za mitihani kwa wale waliopoteza atakuwa amejiondoa mwenyewe katika