MTOTO WA LOWASA NI MTUMISHI HEWA , LOWASA AGEUKA MBOGO .
Waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa amenena baada ya jina la mwanaye kuajwa kwenye orodha ya watumishi waliogushi vyeti vya taaluma iliyokabidhiwa kwa raisi na waziri Kairuki. Listi hiyo ilitolewa na wizara Ofsi ya rais utumishi na menejimenti na utawala bora baada ya Rais Magufuli kuagiza majina hayo yaweke hadharani na kuagiza hazina kutowalipa mshahara wa mwezi huu na watakaokaidi na kuendelea kubakj serikalinj basi miaka saba inawahusu . Katika majina hayo kunajina linalohsishwa na aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowasa jina hilo linasomeka kama Godfey Edward Lowassa kuwa naye ni miongonj mwa wanaosemekana kuwa ni mtumishi hewa na anacheti cha kuchakachua. Jina hilo limetrend sana na leo kupitia ukurasa wake wa twiter Lowassa ameandika haya . "Nitalitolea ufafanuzi jina linalofahamika kama Godfley Ngoyai Lowassa lililopo kwenye list ya wenye vyeti feki muda siyo mrefu "