SERENGETI BOYS YAWACHAPA GABON 2-1
Timu ya Taifa ya vijana U-17 " Serengeti boys" jana meibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Gabon U-17 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa huko Moroco na mchezo huo umepigwa ikiwa ni mchezo wa kujipima kuelekea Gabon kwenye mashindano ya AFCON U-17 . Serengeti Boys imeweka kambi Moroco kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya AFCON U -17 iliyopangwa kufanyika kuanzia mei 14 mwaka huu . Magoli ya Serengeti Boys yalifungwa na Kelvine Nashon na Ibrahimu Abdalah Ally . Mmisanglehotnews.com inaungana na watanzia wote kuitakia timu ya serengezi boys iendelee kujianda vyem ili ikaiwakilishe vizuri nchi katika michuano hiyo.