TETESI : KOCHA MPYA YANGA HUYU HAPA
HABARI ZA MICHEZO : TETESI: KOCHA MPYA YANGA SC Baada ya kuondoka kocha Nabi, klabu ya Yanga imeanza mazungumzo ya mkataba na Miguel Ángel Gamondi. Miguel ni kocha kutoka Argentina anayekinoa kikosi cha Ittihad Tanger (Morocco). Kocha huyo ana uzoefu mkubwa na soka la Afrika kwani kashawahi kuwa kocha mkuu katika klabu za Mamelodi Sundowns, USM Alger, Wydad Casablanca, Platinum Stars na CR Belouzidad. Gamondi pia kashawahi kuwa kocha msaidizi timu ya taifa ya Burkina Faso na Esperance Sportive de Tunis.