Posts

Showing posts from April 2, 2017

SIMBA YASHINDWA KUISHUSHA YANGA KILELENI MWA MSIMAMO WA VPL.

Image
    Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara YANGA jana walicheza mchezo dhidi ya Azam na kuibuka washindi kwa bao moja ,  ushindi ambao uliwafanya waongoze ligi kwa point 56 wakifatiwa na Simba wenye point 55.     Simba wameshuka leo uwanja wa Kaitaba kukipiga na Kagera Sukari na kushindwa kutetea nafasi yao .  Simba walitakiwa kushinda mchezo wa leo ili kurejea kileleni kwa kuwa na point 57 lakini mambo yamekwenda tofauti baada ya kukubali kipigo cha goli 2 kwa 1 kutoka kwa Kagera Sukar .  Mchezo huo ulikuwa mkali na muhimu kwa timu zote kwani Kagera nao walikuwa wakipigania nafasi ya tatu kutoka katika nafasi yao ya nne .   Mpira ulianza kwa kasi kubwa huku Simba wakionyesha nia ya kulisakama lango la Kagera bila mafanikio waliweza kupiga mashuti zaidi ya saba bila kufanikiwa kupata goli hata moja ,  lakini Kagera waliweza kutumia mipira mitatu waliyoipata na kuielekezea golini katika dk ya 28 Mbaraka Yusuph aliweza kuipatia goli Kagera Sukari baada ya kupiga shuti k