MCH. GWAJIMA KAMSAMEHE DIAMOND
Mch. wa kanisa la ufufuo na uzima Mch. Josephat Gwajima leo ameamua kumsamehe mwanamziki Diamond baada ya kuomba msamaha kupitia akaunt yake ya instogram . Mchungaji Gwajima leo aliahidi kumwanika wazi Diamond kuhusu mambo yake ya kujiunga freemason na utoaji wake wa kafara . Lakini Mch. Gwajima alisema jana kupitia akaunt yake ya Instogram alimwomba msamaha . Watu wengi walifunika katika kanisa hilo na wengine kusikiliza kupitia yotube wakitarajia kuwa anafunguka mengi kuhusu Diamond. Lakini karibia na mwisho wa mahubiri yake alidai kuwa bibilia inasema kuwa mtu akiomba msamaha anapaswa kusamehewa hvyo ameamua kumsamehe na kuendelea kumstiri lakini ametoa onto kuwa akiendelea hivyo wiki ijayo atamwanika . Gwajima na Diamond wameingia katika vita baada ya mwanamzi huyo kumwimba mchungaji huyo katika wimbo wake unaoitwa niache nikae kimya .