Posts

Showing posts from April 14, 2017

MCH. LWAKATARE AWA MBUGE WA VITIMAALUMU .

Image
  Mch.  Getrude Lwakatare jana ameteuliwa kuwa mbunge wa viti maalumu. Lwakatare ameteuliwa kuchukua nafasi ya Sophia Simba aliyevuliwa uanachama ndani ya CCM . 

KAGERA SUGAR WAJA NA HII BAADA YA KUNYANG'ANYWA POINT 3 NA KUPEWA SIMBA

Image
 Ikumbukwe kuwa April 2, 2017katika uwanja wa kaitaba ulichezwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar na Simba SC , mchezo uliomalizika kwa simba kupoteza kwa kufungwa goli 2-1  .  Baada ya kufungwa Simba walikata rufaa kwa madai kuwa Kagera walimchezesha Beki wao Mohamed Fakhi akiwa na kadi 3 za njano . Rufaa hiyo simba walishinda na kupewa point 3 na magoli 3 .    Baada ya hapo jana uongozi wa Kagera umeibuka na kudai kuwa wameonewa kwani mohamed Fakhi hakuwa na kadi 3 za njano bali alikuwa nazo 2. Soma barua hiyo

PICHA 8 MAZOEZI YA WACHEZAJI WA YANGA HUKO ALGERIA

Image
Leo nimekusogezea picha 8 za mazoezi ya wachezaji wa Yanga kutoka huko algeria ambako walifanya mazoezi yao ya mwishi mwisho kuelekea mchezo wao wa leo wa marudiano dhidi ya Mc Alger . Yanaga inatakiwa kupata ushindi wa goli moja tu au sare ya aina yoyote ile ili iweze kuendelea mbele katika hatua ya makundi . Ikumbukwe kuwa yanga msimu uliopita iliishia katika hatua ya makundi. 

YANGA WADAI POINT ZAO MBILI NAO SASA

Image
  Baada ya timu ya Simba kupewa point 3 baada ya kagera sugar kumchezesha Mohamed Fakhi ambaye alikuwa na kadi 3 za njano nao yanga wameikumbusha bodi ya ligi kuhusu mchezo waliocheza na mbao fc .  kupitia kwa mjumbe ao a kamati ya utendaji Salum Mkemi amesema kuwa klabu ya yanga haina mpango wa kwenda mahakamani kupinga wapinzani wao kupewa point 3 badala yake leo katika mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya jangwni , Mkemi amesema kuwa hawaezi kwenda mahakamani licha ya kuwa wanachama wao wanaweza kufanya hivyo. Ameelezea kilio chake kwa kamati ya hadhi na sheria za wachezaji kushughulikia malalamiko yao dhidi ya African Lyon kumchezesha Ludovic bila kuwa na uhamisho kamili, kwakuwa mechi yao  na African Lyon iliishia kwa sare ya 1-1 yanga wanapgania kupewa ushindi jambo litakalo waongezea point 2 zaidi .

MANENK YA MANJI ALIPOENDA KUWATEMBELEA YANGA .

Image
     Manji jana alikwenda kuwatembelea wachezaji wa yanga kwa mara ya kwanza toka amalize matatizo yake yaliyokuwa yakimkabili na kusema haya kwa wachezaji na mashabiki wa kikosi hicho .   Manji alisema kuwa "nimewasikia na nayajua matatizo yanayowakabili ,  nawaombeni sana mvumilie kuna mambo nayaweka sawa ndani ya mwezi huu .  Nawaahidi mwezi ujao mtafurahi , nendeni mkacheze tunategemea mtatupa furaha " Manji aliyasema hayo  alipowatembelea katiaka mazoezi yao ya mwisho . 

HARMOROPA KUPIGA SHOW DAR LIVE PASAKA .

Image
Msanii marufu katika mitandao ya kijamii Harmoropa  Anatarajia kutoa show kali siku ya sikukuu ya pasaka katika uwanja wa Dar Live mbagala jijini Dar es Salaam . Meneja na mratibu wa dar live ,  Juma Mbizo alisema kuwa masabiki wa msanii huyo siku nyingi wamekuwa na hamu ya khmuona msanii huyo akipanda jukwaa moja na kulisimamisha kama wanfanyavyo kwenye matamasha mengine.  Mbizo alisema kuwa mbali na msanii huyo kutakuwepo na wasanii wengine wakali kama Juma Nature,  Msaga Sumu,  MC Darada , pamoja na Dula Makabila .   Mapema kuanzia asubuhi kutakuwa na burudani nyingi kwa watoto itakayoongozwa na kundi la Makirikiri kutoka Tanzania.   Kwa upande wake Harmoropa ameahidi kuweka historia katika uh kumbi huo wa Dar Live huku akiwahakikishia mashabiki wake kupata wanachotaka .

MSIMAMO WA LIGI KUU VPL BAADA YA SIMBA KUPEWA POINT 3 ZA KAGERA .

Image
 Jana timu ya Simba ilishinda madai yake ya kupewa point tatu dhidi ya mechi ya kagera waliyokuwa wekundu hao wamepigwa goli 2-1 . Malalamiko hayo ya simba yalikuja baada ya kugunduwa kuwa kagera sugar walikuwa wamemchezesha mchezaji ambaye alikuwa na kadi 3 za njano ambaye ni Mohamed Fakhi.     Sasa Simba wanaongoza ligu wakifuatiwa na Yanga japo wanaongoza kwa michezo mingi. Simba atashuka weekend hii jijini kwanza kucheza na Tot Africa katika uwanja wa CCM Kirumba . 

UWANJA WA CCM KIRUMBA WAPATA KIBALI .

Image
  Mkoani mwanza uwanja wa mpira wa miguu liopo katima mji huo umepata kibali cha kutumika katika michezo ya kimataifa . Fifa   na   Cuf kwa pamoja zimeupitisha uwanja huo kuwa niwakimataifa na kutumika katika michuano yote hata ile ya kimataif . 

RAIS MAGUFULI ALAANI MAUAJI YA POLISI .

Image
  Rais John J P Magufuli amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kuuawa kwa askari wanane walioshambuliwa na ilaha za moto jana eneo la jaribu mpakani wilaya ya kibiti na mkoa wa pwani . Taarifa iliyotumwa na kurugenzi ya mawasiliano ikulu leo inasema askari hao walikiwa wanatoka kubadilishana dolia na amesema wameuawa kwa kushambuliwa wakiwa wamepigwa risasi wakiwa barabarani wakisafiri barabara ya Dar es salaam - Lindi .    Kutokana na tukio hilo raisi amemtumia salamu za rambi rambi mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Ernest Mangu , Family's za askari wote waliouawa , askari polisi wote na watanzania wote walioguswa na msiba huo .  Rais Magufuli amelaani tukio hilo la kuwashambulia askari ambao wanafanya kazi kubwa na muhimu ya kulinda raia  na mali na kuwataka wananchi wote watoe ushirikiano katika kukomesha matukio kama hayo . 

BARAKA DA PRIENCE AWACHANA TEAM KIBA AWAPA MAKAVU.

Image
   Msanii Baraka Da Prience ameibuka na kuwaonya mashabiki wasimpangie cha kufanya katika maisha yake na kusema kuwa wao kinachowahusu ni mziki mzuri kutoka kwake, video na kuwaandalia show nzuri kama mashabiki.      Akizungumza leo amesema hayo baada ya siku kadhaa kushambuliwa na baadhi ya mashabiki ambao walimuita msaliti kwa kuonekana amepiga picha na meneja wa msanii ambaye inaseekana ni hasimu wake mkubwa na msanii Alikiba  ambaye ni msanii mwenzake kutoka katika lebo ya Rock Star 4000.  "Wewe kama ni shabiki wangu wa mziki haimanishi pia kuwa ni shabiki wa maisha yangu binafsi , maisha yangu binafsi muniachie .  Shabiki wewe ninani sasa hadi unipangie maisha , kama mtu niliyepiga naye picha ni mtu tu siyo shetani lakini cha ajabu mashabiki sasa ndiyo wanaonitukana na kuongea hivi na vile wakati uongozi wangu haujasema kama nakosea " alisema Baraka .