Posts

Showing posts from April 21, 2017

STEVE NYERERE ASEMA ni UONGO KUSEMA FILAMU ZA NJE ZINAZUIA ZA KIBONGO KUUZIKA .

Image
             Msanii wa filamu nchini Steve Nyerer ameibuka na kusem kuwa wanaosema kuwa filamu za nje zinasababisha kutokuwa na soko zuri la flamu za ndani ,  ambapo amesema kuwa : "Ni uongo kusema kuwa filamu za nje ndizo zinazuia filamu za ndani (bongo move ) kuuzika ,  ndugu hizi filamu za nje tangu tunazaliwa zilikuwepo , sisi tumemkuta Anold Schwazinger , Rambo na zinauzwa hukohuko Kariakoo kipindi tumewakuta tumechukua Majority yakwao na sisi tumeanza kutengeneza filamu zetu " aliyasema hayo .

RAYVANN ANENA HAYA BAADA YA KUKUTANA NA YONDO SISTER

Image
              Kwa namna ambavyo dunia imekuwa ikiwakusanya watu pamoja na kuwafanya kufika sehemu kwa muda mfupi hasa ukiwa na uwezo wa kufika huko (kifedha ). RayVan nimoja ya watu ambao wanaendelea kutimiza ndoto zao za muda mrefu baada ya kukutana na watu maarufu wa muda mrefu (Legend$) wa mziki wa boringo Yondo Sister na kuandika machache kwenye akaunt yake ya Instagram . "Mungu ni mwema aliyetupa nafasi hii maana haikuwa rahisi kutoka tulipokuwa mtaani mpaka hapa tulipo . Leo nimepata kukutana na mtu mmoja ambaye nilikuwa namshangaa kwenye Tv leo hii naye anasikiliza mziki wangu legend @Yondo_sister pia amesema amefurahishwa sana na winbo  wa Shomwe baada ya Rich Mavoko kumtaja kuwa kiuno kama cha Yondo Sister .  God is Good .

WAZIRI MWAKYEMBE ASEMA YUKO TAYARI KUACHIA UWAZIRI KWA SUALA LA RICHIMOND

Image
       Waziri wa Sana'a, Michezo na Utamaduni Harson Mwakyembe jana alifunguka Bungeni kuwa yupo tayari kuachia nafasi yake ya uwaziri ili aweze kulithibitishia bunge kuwa aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowasa alihusika katika suala la Richimond . Kauli hiyo aliitoa baada ya mbunge wa Arumeru Mashariki (chadema ) Joshua Nassari na mbunge wa jimbo la ubungo (chadema) Said Kubenea kumtuhumu kuwa hakutenda haki mwaka 2008 wakati alipoongoza kamati teule kuchunguza kampuni tata ya ufuaji umeme ya Richmond bila kumhoji Lowasa ambaye alituhumiwa kuhusika . Nasari juzi wakati akichangia bajeti ya Tamisemi  alisema kuwa Mwakyembe amejkataa ripoti ya kuchunguza uvamizi uliofanywa na Makonda katika kituo cha matangazo cha Clouds kwa madai kuwa haikumhoji mkuu huyo wa mkoa ili hali yeye aliendesha kamati ya teule ya bunge ya Richmond kumuondoa madarakani Lowasa licha ya kutokumhoji .