SIMBA YASHINDWA KUISHUSHA YANGA KILELENI MWA MSIMAMO WA VPL.

    Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara YANGA jana walicheza mchezo dhidi ya Azam na kuibuka washindi kwa bao moja ,  ushindi ambao uliwafanya waongoze ligi kwa point 56 wakifatiwa na Simba wenye point 55.
    Simba wameshuka leo uwanja wa Kaitaba kukipiga na Kagera Sukari na kushindwa kutetea nafasi yao .  Simba walitakiwa kushinda mchezo wa leo ili kurejea kileleni kwa kuwa na point 57 lakini mambo yamekwenda tofauti baada ya kukubali kipigo cha goli 2 kwa 1 kutoka kwa Kagera Sukar .  Mchezo huo ulikuwa mkali na muhimu kwa timu zote kwani Kagera nao walikuwa wakipigania nafasi ya tatu kutoka katika nafasi yao ya nne .
  Mpira ulianza kwa kasi kubwa huku Simba wakionyesha nia ya kulisakama lango la Kagera bila mafanikio waliweza kupiga mashuti zaidi ya saba bila kufanikiwa kupata goli hata moja ,  lakini Kagera waliweza kutumia mipira mitatu waliyoipata na kuielekezea golini katika dk ya 28 Mbaraka Yusuph aliweza kuipatia goli Kagera Sukari baada ya kupiga shuti kali nje ya 18 na kumshinda golikipa wa Simba D.  Agey na kutinga wavuni.
  Hadi mapumziko Kagera walikuwa wanaongoza kwa goli 1 -0.

    Mipindi cha pili kilianza kabla hata mchezo haujachangamka dk ya 45 kipindi cha pili E. Christopher aliipatia goli la pili Kagera Sukari kitu ambacho kiliwafanya simba washindwe kuelewa na kuwaacha wakiwa wanatahamaki.  Simba walipambana kiume kwa kulisakama lango la Kagera sukari ,  Mpaka dk ya 66 simba walifanikiwa kupata goli kupitia kwa mchezajj wao  Ruzio .
    Mpaka dk 90 zinamalizika Kagera 2- 1 Simba kwa upande mwingine timu nzima ya Kagera inaweza kumpongeza golikipa wao Juma Kaseja kwa kazi nzuri ya kutoa mikwaju mingi iliyokuwa inaelekezwa langoni na washambuliaji wa Sima walioonekana kuwa na uchungu wa kufunga magoli.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI NA MCHE YANARNDELEA .

BEBI MADAHA NA ISABELA WAHUSISHWA NA KUSAGANA

YANGA KUJA NA JEZI HIZI MSIMU 2017/2018.