VYOMBO VYA HABARI VYAGOMA KUSHIRIKIANA NA MKUU WA MKOA WA DSM PAUL MAKONDA.

   Baada ya mkuu Wa mkoa Wa Dar es Salaam kuvamia Clouds media na kuwalazimisha watangazaji Wa kipindi cha Shilawadu kurusha kipindi kurusha kipindi kinachomhusu Mch. Gwajima kikiwa hakijamaliziwa maandalizi kinyume na taaluma ya habari Jana machi 22, 2017 Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) kimefanya kikao cha maamuzi juu ya suala hilo kuwa hawatotoa ushirikiano wowote na mkuu Wa mkoa huyo ambaye amekuwa akitumia vyombo vya habari katika mikutano yake na shughuli zake za kutimiza majukumu yake.
Pia jukwaa hilo limesema kuwa Kwa mwandishi atakaye husika au kutoa ushirikiano na mkuu Wa mkoa huyo , kitendo chochote kitakachomkuta jukwaa hilo halitahusika Kwa namna yoyote ile .

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI NA MCHE YANARNDELEA .

BEBI MADAHA NA ISABELA WAHUSISHWA NA KUSAGANA

YANGA KUJA NA JEZI HIZI MSIMU 2017/2018.