MECKY MEXIME : SIMBA LAZIMA TUWAFUNGE KAITABA.
Kocha mkuu wa timu ya Kagera Sugar Mecky Mexime amibuka na kusema kuwa wamejipanga kuhakikisha kuwa wanakatisha mbio za ubingwa kwa timu ya Simba S C , kwa kufanikiwa kuibuka na pint 3 katika mchezo wao utakaopigwa siku ya jumatatu pale kaitaba .
Kagera Sugar inatarajia kukutana na Simba april 3 katika uwanja wa kaitaba mjjni bukoba kwenye mchezo ambao unatarajiwa kuwa wa kiupinzani mkubwa kutokana na historia ya timu hizo zinapokutana .
Kagera Sugar ipo nafasi ya nne ya msimamo wa ligi ikiwa na point 42 nyuma ya Azam FC yenye point 44 , huku Simba ikiwa inaongoza ligi ikiwa na point 55 ikiwa imepania kuchukua ubingwa wa ligi kuu msimu huu baada ya kuukosa kwa muda mrefu .
Mexime amesema kuwa timu yake ipo vizuri na imejipanga vizuri kuelekea mchezo huo na kusema hawatakubali kupoteza point tatu zote kwa simba na badala yake anajipanga kuona wanakatisha mbio za ubingwa kwa Simba .
Imeandaliwa na
Misango Samweli
Comments