WAZIRI MWAKYEMBE ASEMA YUKO TAYARI KUACHIA UWAZIRI KWA SUALA LA RICHIMOND

 





     Waziri wa Sana'a, Michezo na Utamaduni Harson Mwakyembe jana alifunguka Bungeni kuwa yupo tayari kuachia nafasi yake ya uwaziri ili aweze kulithibitishia bunge kuwa aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowasa alihusika katika suala la Richimond . Kauli hiyo aliitoa baada ya mbunge wa Arumeru Mashariki (chadema ) Joshua Nassari na mbunge wa jimbo la ubungo (chadema) Said Kubenea kumtuhumu kuwa hakutenda haki mwaka 2008 wakati alipoongoza kamati teule kuchunguza kampuni tata ya ufuaji umeme ya Richmond bila kumhoji Lowasa ambaye alituhumiwa kuhusika . Nasari juzi wakati akichangia bajeti ya Tamisemi  alisema kuwa Mwakyembe amejkataa ripoti ya kuchunguza uvamizi uliofanywa na Makonda katika kituo cha matangazo cha Clouds kwa madai kuwa haikumhoji mkuu huyo wa mkoa ili hali yeye aliendesha kamati ya teule ya bunge ya Richmond kumuondoa madarakani Lowasa licha ya kutokumhoji .

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI NA MCHE YANARNDELEA .

BEBI MADAHA NA ISABELA WAHUSISHWA NA KUSAGANA

YANGA KUJA NA JEZI HIZI MSIMU 2017/2018.