NGOMA NA BOSSOU KUIKOSA MECHI YA LEO DHIDI YA TANZANIA PRISON
Striker Mzimbabwe Donald Ngoma na beki Mtogo Vicent Bossou wameondolewa kwenye orodha ya wachezaji wa timu ya yanga watakao kipiga leo katika uwanja wa taifa katika mchuano wa robo fainali ya kombe la shirikisho .
Wachezaji hawa wameondolewa kutokana na majeraha mbalimbali ambapo Ngoma yeye anahguza Nyonga na Bossou yeye anaugulia goti.
Daktari wa yanga amesema kuwa Ngoma alijitonesha majeraha hayo kwenye mchezo wa marudiano na Mc Alger huko algeria wakati Bosou yeye alipata majeraha kwenye mazoezi wakati wa kujiandaa kwenda Algeria kurudiana na Mc Alger hali iliyosababisha aondolewe kwenye msafara wa timu hiyo .
"Tutawakosa wachezaji wetu Ngoma na Bossou katika mchezo wetu wa kesho (leo) ambapo Ngoma anaumwa nyonga na Bossou anaumwa goti hawa hawatacheza mchezo wa kesho (leo). Bossoututampeleka hospital wakati ngoma anaendelea na matibabu kwani amejitonesha tu hivyo kunauwezekano jumatatu akaanza mazoezi " alisema daktari wa yanga Bavu.
Majeruhi mwingine aliyepo katika kikosi cha yanga ni Justine Zullu ambaye anauguza kidonda cha ugokoni.
Comments