DIWANI APELEKWA POLISI KISA MWENGE

   

     Diwani wa katia ya kitwiru kwa tiketi ya chadema manispaa ya iringa Baraka Kimata ameshikiliwa na polisi kwa muda baada ya kutoa maneno yaliyotafsiliwa kuwa ni ya kashifa kwa mbio za mwenge . Kimata ambaye pia ni katibu mwenezi wa chama cha Chadema Manispaa aliitwa jukwaani kuongea kwa niaba ya chama chake cha Chadema baada ya katibu wa CCM kuongea .

Kimata pamoja na mambo mengine aliyoongea alimalizia kwa kusema kuwa kama CHADEMA ikipewa ridhaa ya kuongoza nchi basi wataupumzisha mwenge wa Taifa . Baada ya hapo wasemaji wote waliofuata akiwemo mkuu wa wilaya ya Iringa na mkimbiza mwenge walimshambulia Kimata na chama chake kwa msimamo huo wa kupinga mbio za mwenge wa Taifa . Baadaye Kimata alikamatwa na kupelekw kituo kikuu cha polisi kuhojiwa na kuachiliwa . Habari kutoka kwa watu wake wa katibu zinasema kuwa Kimata anatakiwa kuandika barua ya kuomba msamaha .

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI NA MCHE YANARNDELEA .

BEBI MADAHA NA ISABELA WAHUSISHWA NA KUSAGANA

YANGA KUJA NA JEZI HIZI MSIMU 2017/2018.