MVUA YAUA WANAFUNZI WAWILI NA KUJERUHI ANNE MKOANI SIMIYU
Wanafunzi wawili wa shule ya msingi Kasoli wakiwa ni ndugu wa familia moja wamefariki dunia huku wengine wanne wakiwa wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta wa kanisa la ACT la kasoli wakiwa wamejikinga na mvua iliyokuwa ikinyesha na kuambatana na upepo mkali .
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu Bonaventure Mshongi amesema ajali hiyo ilitokea tarehe 24 aprili katika kijiji na katia ya Kasoli tarafa ya Mhango wilaya ya bariadi mkoani Simiyu ambapo baadhi ya majeruhi wamelazwa katika hospital teule ya mkoa wa Simiyu na hali zao zinaendelea vizuri.
Comments