HII NDIYO SABABU YA MAALIM SEIF KUTUMBULIWA CUF.

      Baraza kuu la uongozi Taifa (CUF) leo ljmemvua Maalim Seif nafasi yake ya katibu mkuu wa chama hicho na nafasi yake kuchukuliwa na Bi. Magdalena Sakaya .

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo,  mwenyekiti wa CUF anayetambulika na msajili wa vyama vya siasa Taifa Prf. Ibrahim Lipumba amesema baraza hilo limefikia uamzi huo kutokana na sababu mbalimbali ikiwa mojawapo ni kuwa Maalim Seif kutofika ofisini na kutohudhuria vikao vya chama vinavyotambuliwa na katiba ya chama hicho .

"Miongoni mwa ajenda tulizojadili ni kuthibitisha wakurugenzi na manaibu wakurugenzi ,  kupitisha majina ya wagombea ubunge wa bunge la Afrika Mashariki ,  kujaza nafasi za wajumbe wa baraza kuu zilizokuwa wazi , kuunda bodi ya wadhamini , kuunda kamati ya maadili , taarifa ya kesi ,  fedha na taarifa ya hali ya hewa ya kisiasa .
Pia Prf. Lipumba ametangaza nafasi ya majina matatu ya wagombea ubunge katika bunge la umuiya ya afrika mashariki kpitia majna yaliyopendekezwa na kikao cha baraza kuu la uongozi kitaifa kilichokaa march 25 na 26 mwaka huu.
Majina matatu yaliyoteuliwa na baraza kuu la uongozi kitaifa ni Sonia Magogo , Mohamed Habibu Mnyaa na Thomas Malima mmoja kati yao akitoka serikali ya mapinduzi zanzibar.  Mbali na hapo Lipumba amemtangaza Bwn.  Abdul Kambaya kuwa mkurugenzi wa habari, uenezi na mahusiano ya umma ambapo awali hakuwa mkurugenzi wa habari, uenezi wa habari , uenezi na mahusiano ya umma.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI NA MCHE YANARNDELEA .

BEBI MADAHA NA ISABELA WAHUSISHWA NA KUSAGANA

YANGA KUJA NA JEZI HIZI MSIMU 2017/2018.