SIMBA WAMALIZANA NA WACHEZAJI WAO HAWA.

             Mabosi wa simba wameangalia nyota kadhaa wakali wanaomaliza mikataba yao katika kikosi cha watani zao yanga na kubaini kuwa wananafasi ya kuipiga bao na kujitengenezea ufalme .
Simba inaonekana kujipanga mapema ili kuweza kutawala soka la Tanzania bara kwani katika kikosi chao cha kwanza ni wachezaji wawili tu wanaomaliza mkataba msimu huu ambao wanalazimisha uondoka tofauti na watani zao ambao karibu kikosi kizima wachezaji wanaomaliza mkataba .
Nyota wa simba ambao wanaomaliza mkataba na wameshinikiza kuondoka nipamoja na Ibrahim Ajibu & Jonas Mkude ambaye hata hvyo mbadala wake ameshapatikana .
Nyota anayeandaliwa urithi mikoba ya Mkude ni Mghana James Kotei ambaye tayari kashaanza kupata nafasi katika kikosi cha kwanza .
Nyota wengine ambao tayari walikuwa wanaomaliza mikataba yao na tayari wameshaongezewa ni Mohamed Hussein 'Tshabalala' na Abud Banda aliyetayari katika mazungumzo ya kuongeza mkataba.
Nyota wa kikosi cha kwanza wanaomaliza mikataba yao nipamoja na mabeki Haji Mwinyi na Vicent Bosou , viungo ni Haruna Niyonzima na Thaban Kamusoko pamoja na mshambuliaji Donald Ngoma .

Makamu wa raisi wa simba Geofrey Nyange 'kaburu' amesema kuwa wamehakikisha kuwa wanaendelea kubaki na kikosi chao hasa cha kwanza kwani wengi wao bado ni vijana wenye uwezo wa kucheza kwa muda mrefu .  Kaburu alisema kuwa hata wachzaji ambao mikataba yao inamalizika bado wapo katika mazungumzo nao kuona kama kuwabakisha inawezekana kwani ni juhudi za kuendela kuwa na kikosi kilicho imara hata kwa msimu ujao .

"Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwabakisha wachezaji muhimu katika kikosi ,bado tupo kwenye mazungumzo na wengine ambao walionyesha nia ya kutka kuondoka . Nia yetu ni kuhakikisha wachezaji wote muhimu wanabaki" alisem Kaburu.

         MO ATIA CHACHU .
   
        Katika hatua nyingine ,  Kaburu alisema kuwa hapo mambo matatu ambayo yamewafanya mpaka sasa kuwa kileleni mwa ligi kuu Tanznia Bara iliyobakiza michezo sita kumalizika ,  alisema kuwa Mohamed Dewji ni miongoni mwa sababu ikiwa amechukua jukumu la kuwalipa mishahara wachezaji kuanzia mwezi septemba mwaka jana .

"Wanachama wamekuwa pamoja , kwa wakati wote wamekuwa wakitoa michango kuhakikisha wachezaji wanapata posho nzuri na wanasafiri vizuri .  Viongozi pia tumekuwa makini kuhakikisha tunawaunganisha wanachama na kutumia vizuri michango " alisema .

              By : misango samweli .


Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI NA MCHE YANARNDELEA .

BEBI MADAHA NA ISABELA WAHUSISHWA NA KUSAGANA

YANGA KUJA NA JEZI HIZI MSIMU 2017/2018.