UHAKIKI WA VIGOGO WENYE VYETI FEKI .

       Ikulu yamutwisha mzigo waziri. 
  Wakati uhakiki wa vyeti kwa wathmishi wa uma ukikamilika leo ,  ikulu imemtwisha mzigo waziri wa Nchi, Ofisi ya rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) ,  George SimbaChawene kuwa ndiye mhusika wa suala hilo .
  Kwa mjibu wa tangazo lililotolewa march 20 mwaka huu na katibu mkuu Ofis ya Rais ,  Manejiment ya utumishi wa uma na utawala bora Dk.  Laurian Ndumbalo ,  uhakiki wa vyeti vya elimu na taaluma pamoja na namba za mitihani kwa watumishi wa umma ulioanza march 12 mwaka jana utakamilika rasmi leo.
   Katika tangazo hilo Dk.  Ndumbalo amesema kuwa uhakiki huo haujalenga kumkomoa mtumishi wa umma bali kuhakikisha kuwa na watumishi wenye sifa zinazotakiwa kitaaluma na kitaalamu ili kutoa huduma zilizo bora na kwa weledi kwa wananchi.
  "Serikali inasisitiza kuwa mtumishi wa umma atakayeshindwa kutumia muda uliotolewa ili kuwasilsha nakala za vyeti au namba za mitihani kwa wale waliopoteza atakuwa amejiondoa mwenyewe katika ajira serikalini." Linaeleza tangazo hilo ambalo Frolence Temba mkuu wa kitengo cha mawasiliano ,  serikalini Ofisi ya Rais Utumishi alilithibitishia Nipashe kuwa ni lao .

   Alipoulizwa na rais kuwa uhakiki huo unawahusu pia wateule wa rais ,  Temba alisema ni kwa watumishi wote wa umma , lakini akadai kuwa vyeti vya watehle wa rais vinahaikiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI .
  Simbachawene alipotafutwa kuzungumzia suala hilo , alidai masuala ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma wakiwemo wateule wa Rais unafanywa na Wizara ya Nchi Ofisi ya menejiment ya utumishi wa umma na utawala bora .



             Imeandaliwa na Misango Samweli 

Kwa matangazo tuma ujumbe whatsap 
        0625954293

 "

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI NA MCHE YANARNDELEA .

BEBI MADAHA NA ISABELA WAHUSISHWA NA KUSAGANA

YANGA KUJA NA JEZI HIZI MSIMU 2017/2018.