YANGA KESHO KUKAA KILELENI LIGI KUU VPL .
Simba wameshindwa kutamba katika mchezo wao dhidi ya Mbeya City leo baada ya kulazimishwa kutoa suluhu ya 2-2 uwanja Wa Taifa leo . Kesho timu ya YANGA itashuka dimbani kumenyana na MTIBWA SUGAR , endapo Yanga watashika mchezo huo watakaa kileleni mwa ligi kuu ya VPL ambapo watakuwa na point 55 sawa na SIMBA lakini wataongoA Kwa tofauti ya Magoli kwani watakuwa na magoli mengi ikiwa wamecheka na nyavu Mara 49 huku simba wamecheka na nyavu hizo Mara 38 . Yanga watakuwa wageni kesho katika uwanja Wa Jamhuri Morogoro wakikaribishwa na Mtibwa Sugar .
Comments