YANGA YAPATA MTIHANI KUELEKEA MCHEZO NA AZAM FC .
Kuelekea kwenye mchezo wa kesho jumamosi dhidi ya Azam FC , benchi la yanga lipo kwenye mtihani mzito juu ya kupanga kikosi chake kitakachokuwa na uhakika wa kupata ushindi .
Yanga haitakuwa na huduma ya mabeki wake Elvine Yondan, Ramadhan Kessy ambao watajkosa mchezo huo kutokana na kuwa na kadi tatu za njano .
Pia yanga itamkosa mshambuliaji wake mrundi Hamis Tambwe ambaye anauguza majeraha , kocha wa timu hiyo Lwandamina alisema hayo kuwa hiyo ni changamoto kubwa kwa benchi lake lakini wanafanya kila linalowezekana ili kupata ushindi huo wa point tatu.
"Bado kuna wachezaji wengine ambao wanaweza kucheza na kuziba nafasi hizo , mambo kama hayo yanatokea kwenye timu huwezi ukawa na wachezaji wote wakawa vizuri bila majeraha kwenye mechi zote " lisema Lwandamina .
Lwandamina alisema kuwa habari nzuri kwao ni kurejea kwa mshambuliaji wao Donald Ngoma ambaye amekuwa na majeraha ambaye jana alitarajiwa kuanza mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake .
Kocha huyo juzi alitumia muda wa saa mbili kufanya mazoezi ya peke yake huku akikimbia na kuzunguka uwanja huku akitumia muda wa saa moja kufanya mazoezi ya viungo .
BOSOU HAKIJAELEWEKA
Beki huyo aliyekwenda nchinj Togo kuitumikia timu yake ya Taifa , alikuwa akitarajiwa kutua nchinj jana kama yanga tu wangekuwa wamemtumia tiketi ya ndege yeye na mke wake . Mpaka kufikia juzi jioni Bosou alikuwa hajatumiwa tiketi.

Comments