BARAKA DA PRIENCE AWACHANA TEAM KIBA AWAPA MAKAVU.
Msanii Baraka Da Prience ameibuka na kuwaonya mashabiki wasimpangie cha kufanya katika maisha yake na kusema kuwa wao kinachowahusu ni mziki mzuri kutoka kwake, video na kuwaandalia show nzuri kama mashabiki.
Akizungumza leo amesema hayo baada ya siku kadhaa kushambuliwa na baadhi ya mashabiki ambao walimuita msaliti kwa kuonekana amepiga picha na meneja wa msanii ambaye inaseekana ni hasimu wake mkubwa na msanii Alikiba ambaye ni msanii mwenzake kutoka katika lebo ya Rock Star 4000.
"Wewe kama ni shabiki wangu wa mziki haimanishi pia kuwa ni shabiki wa maisha yangu binafsi , maisha yangu binafsi muniachie .
Shabiki wewe ninani sasa hadi unipangie maisha , kama mtu niliyepiga naye picha ni mtu tu siyo shetani lakini cha ajabu mashabiki sasa ndiyo wanaonitukana na kuongea hivi na vile wakati uongozi wangu haujasema kama nakosea " alisema Baraka .
Comments