DARASA KUJA UPYA ZAIDI ACHANA NA WIMBO WA MZIKI HII NI KALI ZAIDI
Mashabiki wengi nchini wanataka kujua kuwa msanii Darasa atakuja na ngoma gani mpya baada ya kukaa chimbo kwa muda mrefu na bado yuko na tour zake Rwanda na Burundi na baada ya hapo ataachia ngoma yake mpya .
Director Hanscana ambaye kwa sasa anafanya kazi na rapa huyo amefunguka juu ya ujio wa rapa huyo ambaye bado anatamba na ngoma yake ya Muziki .
"Sisi tumejiandaa vizurj kwa sababu tunajua mashabiki wanataka nini " alisema Hanscana
"Maandalizi ni makubwa sana nikama tunaandaa maraisi watano wa nchi , kwahiyo tumejipanga vizuri kuhakikisha jamaa anarudi vizuri kwenye game" alisema Hanscana .
rapa huyo alikuw aachie wimbo mpya mwezi huu lakini ameshindwa kutokana na tour yake ya kimataifa . Video ya wimbo wa muziki ya rapa huyo mpaka sasa imeangaliwa mara 7056225 katika mtandao wa youtube kwa kipindi cha miezi mitano .
Comments