GWAJIMA AMSHAURI MAFUFULI PA KUMPELEKA MAKONDA.
Mch. Gwajima amesema kuwa bora mkuu wa mkoa wa DSM Paul Makonda apelekwe nje na akawe balozi kuliko kumwacha hapa nchini watamgawana .
Gwajima kuhusu makonda leo kwenye ibada ya jumapili tarehe 9, April amesema :
"Kwanza huwa najiuliza kuwa rais Magufuli akjmtoa leo Makonda kmataenda wapi ? Lakini naushauri mmoja ampeleke kwenye balozi zetu nje ya nchi kwani akimuacha hapa watu watamugawana . Na akiendelea kumuacha ipo siku atafanya vitu vya ajabu na kuliaibisha taifa , kwanza mimj ningekuwa MAKONDA ningeshaondoka siku nyingi . Na hayo mambo ya ajabu yatakuja kutokea bado Niko hai " alisema Gwajima .
Pia Gwajima amesisitiza kuwa ataendelea kuliongelea suala la vyeti na makonda na kuachana na mambo mengine .
Comments