HOTUBA YA MHE. ZITO KABWE LEO BUNGENI.

    Hali ya uchumi ni mbaya watanzaia wamepoteza matumaini. 

[Sehemu kwanza ya haotuba ya Mh. Zuberi Zitto kabwe (mb) kuhusu mwelekeo na kazi za serikali kuhusu badjeti ya ofisi ya Waziri mkuu ya mwaka 2017/2018 ]

       Mhe.  Spika. 
    Tangu mwezi Novemba 2015 serikali yetu ilipata uongozi mpya iliyoanza kwa kasi mpya hasa katika masuala ya kupambana na rushwa, ufisadi na kuongeza mapato ya serikali. Wananchi walikuwa na matumainj makubwa sana hasa kuhusu ufanisi wakazi serikali uliboleka .

  Bahati mbaya leo tunapokutana kujadili utendaji wa serikali wa mwaka uliopita  na kupanga bajeti ya mwaka ujao matumaini hayapo tena . Kuna hali kubwa ya kukata tamaa kwa wananchi.

  Maeneo mengi ya nchi kuna uhaba wa chakula na badala yake serikali hasa raid kuwa matumaini kwa wananchi akiwa Confoter in Chief , kumekuwa na maneno makali ya kuwakatisha tamaa wananchi . Bei za vyakula nchini zimepanda mno kiasi kwamba wananchi wanashindwa kumudu ili waweze kufanya biashara za kukuza uchumi.
Taarifa za serikali kupitia ripoti za Benki kuu zilizopo kwenye tovuti ya serikali juu ya uchumi wa nchi yetu (Qualitely Economic Review na Monthly economic review ) kwa mwezi wa Disemba 2016 zinasema kuwa kuna mfumko mkubwa sana wa bei za vyakula , hasa chakula kikuu cha watanzania -Mahindi ,  ambapo bei ya chakula hicho kikuu cha watanzania imepanda kwa 30% na kupandisha mno ghalama za maisha kwa wananchi nchi nzima .

    Leo bei ya kilo ya mahindi nchi nzima iko sawa na bei ya kilo ya mchele kwenye miji mbalimbali nchini, sukari bei juu , mafuta ya kupikia bei juu n k.
Kwa wakazi wa mjini hata gesi ya kupikia majumbani imepanda wananchi wamerudia matumizj ya mkaa tujiandae na uharibifu wa misitu nchini .
Jana ofisi ya takwimu ya aifa imetoa takwimu kuwa mfumko wa bei imepanda kwa kasi na sasa umefika 6. 4 % kwa mwaka unaoishia March.  2017.

Ibara ya 20 ya hotuba ya waziri mkuu iliyosomwa bungeni inaoyesha kuwa mfumko wa bei ni 5. 2 % ?kwani wameonyesha takwimu za mwezi desemba 2016.

Ukuaji wa sekta binafsi umedorola na kushuhudia biashara maelfu kwa maelfu zikifungwa  na kusababisha ajira nyingi zikipotea na kutengeneza uhaba wa ajira kutengenezwa.

Katika ibara ya 26 ya hotuba ya waziri mkuu inaonekana kuwa ajira 418000 zilizalishwa mwka 2016/2017. Lakini waziri mkuu hakulieleza taifa kuwa hivi sasa watanzania 1. 6m wanaingia kwenye soko la ajira kila mwaka . Pia waziri mkuu hakulieleza taifa kuwa ni ajira ngapi zimepotea kwa viwanda  kufungwa na kupunguza uzalishaji na biashara kufungwa .
Manispaa ya ilala peke yake imefunga biashara 2900 na hivyo kupoteza chanzo cha mapato . Lakini hata mikopo ya kibank kwa makampuni bianfsi imepungua mno ikiwa ni kiashiria cha mdororo wa sekta binafsi .

Matamko ya viongozi wakuu wa serikali kuhusu mwelekeo wa uchumi yanatuma ujumbe basi kuhusu uwekezaji wa mitaji nchini, na hivi sasa kila mwekezaji kwenye macho ya serikali anaonekana nimpiga dili . Juhudi zote za kuhamasisha uwekezaji nchini zilizofanywa tangu awamu ya tatu zimefutwa katika mwka mmoja tu wa awamu ya tano , hali hii ni yakusikitisha sana .

Tatizo lingine kubwa ni suala la ajira , ukiondoa ajira zilizopotea kwa mdororo wa sekta binafsi , Lakini pia hakuna ajira mpya tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani . Vijana mbalimbali waliomaliza masomo yao ya ualimu, utabibu , maafisa kilimo , uvuvi na ufugaji bado wapo mitaani bila ajira kwa mwaka sasa . Hata walioajiliwa mwanzoni ajira zilisitishwa kwa kisingizio cha uhakiki wa watumishi hewa .

Yote hayo yana athari kwa uchumi wa nchi, yamepunguza kipato kwa wananchi , yamechangia maisha magumu na yamefuta matumaini waliyokuwa nayo watanzania na yamewakatisha tamaa. Bunge letu linawajibu wa kuhakikisha serikali inarekebisha hayo.




                                          Imeandaliwa na

                                     Misangle S  Masanger

                                            Whatsap
       
                                           0625954293

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI NA MCHE YANARNDELEA .

BEBI MADAHA NA ISABELA WAHUSISHWA NA KUSAGANA

YANGA KUJA NA JEZI HIZI MSIMU 2017/2018.