KWA MWENDO HUU SINGIDA UNITED LAZIMA WAFANYE MAAJABU KATIKA LIGI KUU VPL 2017/2018.


        Klabu  ya Singida United leo itafanya Suprise katika kuendeleza usajili wao ambapo watatangaza mchezaji mwingine na kusisitiza kuwa nafasi zote saba wao watazijaza msimu huu lengo ni kuwa na kikosi imara katika usiriki wao katika ligi kuu baada ya muda mrefu bila kusiriki. Na saprise ya wachezaji wapya watakaowatangaza ni kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kwa Uganda, Rwanda na Burundi na wote ni wachezaji kutoka timu zao za Taifa sasa usije shangaa akawa ni Mnyarwnda Iranz Jean Claude wa APR.
      Na hii ni baada ya kuwasajili wazimbabwe kiungo Elisha Mroiwa mwenye miaka 27 , Wisdom Mtasa miaka 22 ambaue ni mshambuliaji wa Taswadaza Kutinyu. Katibu mkuu wa Singida United Abdurahman Sima aliweke wazi nafasi saba watakazpsajili kuwa nibeki wa kulia, kushoto, kati, kiungo mkabaji , kiungo mshambuliaji pamoja na mastriker namba tisa na kumi na wote lazima wawe wanatoka timu zao za Taifa
"Kesho (leo) tutatangaza usajili wetu mwingine wa wachezaji ambao watakuwa wanatoka katika ukanda wa afrika mashariki katika nchi tatu Rwanda, Burundi na Uganda tunachofanya sasa ni kumalizia michakato iliyobaki.  Alisema Sima.
 " tutasajili wachezaji saba na wote wa kigeni tofauti na tuivyopanga awali lengo likiwa ni kutengeneza timu  itakayokaa kwa muda mrefu na kuzoeana ndiyo mana tunawapa mikataba ya miaka miwili na si chini ya hapo . Usajili huo ni mipango ya kocha Hans Pluijm na benchi la ufundi  licha ya kuwa safari tumekuwa tukiwasiliana naye mara kwa mara ,  alisema Sima.
     
   Singida imekuwa kimya kwa kipindi chote cha usajili na wachezaji wao wa ndani na Sima amesema kuwa  "kwa wachezaji wa ndani zoezi litafanyika hapo badae, inakuwa ngumu kwa sababu ligi bado inaendelea " alisema Sima.

                           Imeandikwa na Misango samweli

                                  Whatsap      No.
                         
                                      0625954293

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI NA MCHE YANARNDELEA .

BEBI MADAHA NA ISABELA WAHUSISHWA NA KUSAGANA

YANGA KUJA NA JEZI HIZI MSIMU 2017/2018.