MESSI AWAUA REAL MADRID NA KUFIKISHA MABAO 500 AKIWA B
Lione Messi "la Pulga" alikuwa na usiku mzuri sana baada ya kuwa stari wa mbele kuiangamiza Real Madrid katika uwanja wao wa nyumbani Santiago Bernabou .
Real Madrid ndiyo waliotangulia kuliona lango la barcelona katika dk ya 28 tu kupitia kwa Casemiro kabla ya Lionel Messi kuwasawazishia barcelona na kwenda mapumziko kwa safe ya 1-1.
Kipnd cha pili barcelona walipata bao la pili kupitia kwa Ivan Ractic na wakati Madrid wakiwa katika harakati za kusawazisha walipata tatizo baada ya mchezaji wao Sergio Ramos kupata kadi nyekundu .
Kadi nyekundu haikuwazuia Madrid kulisakama lango la barcelona na katika dk ya 86 kupitia kwa James Rodriguez aliwasawazishia Madrid huku akiwa anatokea benchi.
Hadi inafika dk 90 matokeo yalikuwa 2-2 huku mashabiki wakiamini kuwa mchezo huo ungemalizika kwa sare ya 2-2 , Lionel Messi katika dk za nyongeza akikokota mpira na kuifungia barcelona goli la tatu .
Messi ambaye amekuwa kinara wa El Classco kwa muda mwingi hilo lilikuwa goli lake la 500 kwa timu yake ya Barcelona na matokeo hayo yamewafanya barcelona kuwa na point sawa na madrid huku Barcelona wakiongoza ligi kwa tofauti ya maswali .
Comments