MWANJALE AANZA MAZOEZI CHINI YA UANGALIZI WA DAKTARI.
Beki wa kikosi cha Simba Method Mwanjale ameanza mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa Daktari. Mwanjale aliumia na amekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi miwili sasa . Sasa ameanza mazoezi mepesi na Mratibu wa Simba Abasi Ally "Gazza" amesema kila kitu kinafanyika chini ya uangalizi .
"Daktari ndiye anasimamia kila kitu , hivyo anajua nini anatakiwa kufanya ingawa ameanza mazoezi mepesi chini yake " alisema Gazza
Mwanjale yuko Morogoro na kikosi cha simba ambacho kimeweka kambi huko kujiandaa na mechi dhidi ya Azam kwa ajili ya nusu Fainali ya kombe la Shirikisho .
Simba imekuwa ikiyumba katika safu yake ya ulinzj kutokana na kumkosa Mwanjale raia wa Zimbabwe ambaye amkuqa ni tegemeo kubwa katika kikosi hicho .
Comments