RAIS MAGUFULI AKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI (TUCTA)
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk . John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) ikulu jijini Dar es Salaam .
Pamoja na mambo mengine viongozi wa TUCTA wamemhakikishia kuwa vyama vya wafanyakazi vitafanya kazi bega kwa bega na serikali katika kusimamia haki na uwajibikaji wa wafanyakazi . Mhe. Magufuli amesema serikali inawapenda na ipo tayari kuboresha masilahi yao lakini amewataka wafanyakazi kutanguliza maslahi ya Taifa .
Comments