RAIS MAGUFULI ALAANI MAUAJI YA POLISI .
Rais John J P Magufuli amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kuuawa kwa askari wanane walioshambuliwa na ilaha za moto jana eneo la jaribu mpakani wilaya ya kibiti na mkoa wa pwani .
Taarifa iliyotumwa na kurugenzi ya mawasiliano ikulu leo inasema askari hao walikiwa wanatoka kubadilishana dolia na amesema wameuawa kwa kushambuliwa wakiwa wamepigwa risasi wakiwa barabarani wakisafiri barabara ya Dar es salaam - Lindi .
Kutokana na tukio hilo raisi amemtumia salamu za rambi rambi mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Ernest Mangu , Family's za askari wote waliouawa , askari polisi wote na watanzania wote walioguswa na msiba huo .
Rais Magufuli amelaani tukio hilo la kuwashambulia askari ambao wanafanya kazi kubwa na muhimu ya kulinda raia na mali na kuwataka wananchi wote watoe ushirikiano katika kukomesha matukio kama hayo .
Comments