VITA MPYA YA DIAMOND NA GWAJIMA .
Mch. Gwajima amemuumbua mwanamziki wa kizazi kipya Diamond Plutinum na kusema kuwa msanii huyo ni mwanachama wa freemason na kusema kuwa kama anakataa siyo kweli basi msanii huyo aibuke na kusema ukweli .
Mchungaji huyo alisema kuwa leo katika solo lake atampiga mtu ambaye yupo katika kundi la wanaotoa kafara freemason.
"Leo kuna MTU nitampiga katika somo letu la wanaotoa kafara freemason , kabla hujaniimba uwaze mara mbili (2).
Nitampiga mtu na nitatoa ushahidi wa alibmvyojiunga na freemason (wa video na picha ). Anapata wapi ujasiri wa kuniongea ? " alisema Gwajima siku chache baada ya msanii Diamond kuachia wimbo aliomuimba Mch. Gwajima siku chache baada ya kuuachia wimbo unaokwenda kwa jina la Acha nikae kimya , wimbo ambao umezua gjmzo katika mitandao ya kijamii.
Comments