YANGA YAPAA KILELENI MWA LIGI KUU VPL.

     Yanga imekaa kileleni mwa ligi kuu leo baada ya kuibuka na ushindi wa goli moja . 
   
     Ligi kuu VPL leo imeendelea kwa michezo miwili , macho na masikio ya watanzania wengi yalikuwa katika mchezo uliopigwa jijini Dar es Salaam ambapo timu za YANGA na AZAM FC zilikuwa zinaonyeshana ubabe .
   Yanga alikuwa mwenyeji katika mchezo huo ,  mchezo ulianza kwa timu ya Yanga kuzidiwa na AZAM kwa kila namna , wachezaji wa Azam walionekana kuwa vizuri zaidi tofauti na wale wa Yanga .  Mpaka timu hizo zinaenda mapumziko zilikuwa sare ya 0-0 .
  Baada ya mapumziko kuisha timu hizo zilirejea uwanjani kwa kila moja kutafuta goli la kuongoza ,  mpaka dk ya 69 hakuna timu iliyokuwa mbele ,  dk 70 mshambuliaji Obrey Chirwa aliipatia goli Yanga baada ya kumalizia pasi maridhawa iliyopigwa na Haruna Niyonzima na kufanikiw kuwatoka mabeki wawili wa Azam .
  Ushindi huo unaipekeka kileleni Yanga kuongoz kwa point moja mbele ya Simba ambayo itashuka kesho kuchuana na Kagera Sugar mjini Kagera .

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI NA MCHE YANARNDELEA .

BEBI MADAHA NA ISABELA WAHUSISHWA NA KUSAGANA

YANGA KUJA NA JEZI HIZI MSIMU 2017/2018.