YANGA YAZDI KUPATA MAMILIONI.
Ikiwa ni siku moja baada ya uongozi wa yanga kuanza harambee ya ukusanyaji wa fedha kwaajili ya kuisaidi klabu hiyo, tayari klabu hiyo imeanza kupokea fedha mbalimbali kutoka kwa wadau na mashabiki wa soka mbalimbali.
Juzi uongozi wa yanga ulizindua harambee kwa ajili ya watu mbalimbali kuichangia fdha timu hiyo ili iweze kuendelea na shughuli zake za kimaendeleo zoezi ambalo limeanza kwa kishindo kikubwa .
Katibu mkuu wa klabu Charles Boniface Mkwasa" amesema fedha hizo zitakuwa ni kwaajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo kuwalipa mishahara wachezaji wake ambao wanadai mwezi uliopita na ujao .
Mkwasa amesema anashukuru sana kwakuwa zoezi la uchangishaji limepokelewa vizuri sana na wanachama kwani wenye mapenzi wameanza kujitoa kwa hali na mali .
"Klabu inathamini mtu kwa kiwango chochote anachotoa , pia tunatanguliza shukrani za dhati na kutambua umuhimu wa kila mmoja katika mchakato huu." alisema Mkwasa.
Alisema pia uongozi utakuwa unatoa taarif aya mapato yote yanayopatikana kutoka kwa wanachama wote kila wiki ili wanachama waweze kufahamu mwenendo wa michango yao kwa ujumla .
Aidha, Mkwasa alisema kuwa zoezi hili litafanyika kwa muda wa miezi miwili , huku akitarajia upata fedha ambazo zitatosha kuwalipa wachezaji pamoja na mambo mengine na shughuli zake ndani ya klabu hiyo .
Yanga ambayo ipo katika nafasi ya pili ikiwa na point 56 iko katika harakati za kutetea ubingwa wao na wamepata nguvu hasa baada ya klabu ya Simba kunyang'anywa point walizokuw wamepewa kutoka klabu ya Kagera Sugar
Comments