MALALAMIKO YA SIMBA KUHUSU POINT 3 ZA MCHEZO WAO NA KAGERA YATUA FIFA.
Makamu wa raia wa klabu ya Simba Geofley Nyange "Kaburu" amesema tayari wametuma barua ya malalamiko yao FIFA kuhusu point 3 walizonyang'anywa na TFF baada ya Kagera Sugar kumtumia mchezaji Mohamed Fakh aliyekuwa na kadi 3 za njano walipocheza mechi dhidi yao ya ligi huko bukoba .
Kaburu amesema kuwa barua yao ya malalamiko imepokelewa na FIFA wanachosubiri ni uamzi wa shirikisho hilo la mpira dunuani .
"Tumeshatuma malalamiko yetu FIFA na tumeainisha kuwa tunataka nini , nisiwasemee mana wao watasoma na wataamua na kutujulisha walichoamua " amesema Kaburu alipokuwa akizungumza na Clouds FM katima kipindi cha Sports Extra.
Kwa sasa Simba inapoint 65 point tatu nyuma ya Yanga na ikiwa timu zote zimebakiza mchezo mmoja . Ikiwa simba watapewa point hizo wanaweza kuwa katima nafasi nzuri zaidi ya kuchukua ubigwa kwani watakuwa wakiiombea Yanga ipoteze katima mchezo wake wa mwisho huko mwanza dhidi ya Mbao huku wao wakitakiwa kushinda mchezo wao dhidi ya Mwadui.
Comments