KOSA WALILOFANYA SIMBA KUELEKEA DAR DERBY YA JUMAMOSI HII.
Mwenyekiti wa klabu ya Simba wa zamani Ismail Rage amesema yalifanyika makosa makubwa sna kuwaachia Hamis Tambwe na Ibrahimu Ajibu ambao wote walipotoka klabu ya Simba walijiunga na Yanga.
Akizungjmza Rage amesema kuwa vijana wangu walifanya makosa kumwachia Ibarahim Ajibu "Lazima niseme ukweli kuwa vijana wangu walifanya makosa kumwachia Ajibu ingawa inawezekana alikuwa na matatizo yake kwani nikijana mzuri , kinachotakiwa ukiwa kiongozi ni lugha nzuri ya kumvutia kila mchezaji "
Mchezaji mzuri kama Ajibu au Tambwe ilikuwa ni makosa kumwachia kwenye klabu ya Simba kwa kuwa ameondoka na kwenda mikononi mwa watu . Siku zote watu ambao wanatoka Simba na kwenda mikononi mwa Yanga , basi tena wanapoteza ile thamani yao hata iwe ulikuwa mzuri kiasi gani .
Ajibu amekuwa na mchango mkubwa kwa klabu ya Yanga tangu asajiliwe , amekuwa na magoli matano mpaka sasa katika mashindano ya VPL. Tambwe pia amekuwa akiendelea kufanya vyema tangu ajiunge na yanga baada ya kutemwa na Simba na amekuwa akiwafunga kwenye mchezo wa watani wa jadi "alisema Rage .
Comments