MVUA ZILIZONYESHA DAR ES salaam ZALETA HASARA KWA WAKAZI WA JIJI HILO
Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam zimeendelea kuwa kero kwa wakazi wa jiji hilo kwa kusababisha watu kukimbia makazi yao na hasara kuwa kutokana na maji kujaa ndani .
Na inahofiwa mtu mmoja kupoteza maisha kutokana na mvua hizo ambazo zimepelekea hata usafiri kuwa wa shida katika jiji hilo .
Mamlaka ya hali ya hewa imesema kuwa mvua hizo zimevunja rekodi ya tangu kuanzishwa kwa baadhi ya vituo hivyo vya ufuatiliaji wa hali ya hewa miaka ya 1964
Comments