KICHUYA AIWEKA SIMBA KILELENI MWA VPL SIMBA IKISHINDA GOLI MOJA
Goli pekee la Kichuya limeifanya Simba kurudi kileleni mwa ligi kuu ya VPL baada ya kuifunga Mbeya City kaika chezo uliomalizika hii jioni ya leo .
Kabla ya mchezo huo Simba ilikuwa nyuma kwa point moja nyuma ya yanga na Mtiwa amazo zilitoka sare katika michezo yao ya jana lakini ilikuwa imezidiwa na Azam ambayo ilishida mchezo jana dhidi ya Ruvu Shooting.
Ushindi wa Simba wa leo umeipa point 3 na kufanya kuwa na point 19 sawa na Azm lakini Sinba inaongoza kwa kuwa na wastani mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa .
Simba imeshinda mechi 3 kati ya 5 ilizocheza na mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine , Mbeya kabla ya mchezo wa leo simba ilikuwa imeshinda mechi 2 kati ya nne huku mchezo mmoja wakitoka sare na mwingine walipoteza.
Kichuya anafikisha magoli matano (5) sawa na Ibrahimu Ajibu wa yanga huku wakiwa wamezidiwaana Mohamed Rashidi wa Tanzania Prison mwenye magoli sita (6)huku wakiwa wamezidiwa na kuongozwa na Emanuel Okwi wa Simba mwenye magoli tisa(9).
Mbeya City imepoteza mchezo wa pili kati ya michezomitano waliyocheza katika uwanja wa Sokoine yaani nyumbani , mchezo mwingine waliopoteza wakiwa nyumbani ilikuwa dhidi ya Ndanda .
Simba imeshinda mechi yake ya pili nje ya uwanja wa uhuru ambao ndiyo uwanja wao wa uhuru.
Comments