KUELEKEA MADRID DERBY:WANDA METROPOLITANO KUANDIKA HISTORIA LEO HII

   

    Estadio Wanda Metropolitan ndiyo uwanja ambao Derby ya Madrid I itapigwa Leo hii na itakuwa uwanja Wa 16 kuwahi kutumika katika michezo ya aina hii ya mahasimu Wa jiji la Madrid.

  Ni ukurasa Mpya Wa ukurasa uliodumu Kwa zaidi ya karne Kwa vilabu hivi vya mji Wa Hispania .
Yangu vilabu hivi vilipoanzishwa ,mechi kubwa kati ya Athletics na Real Madrid zimechezwa katika maeneo yote yenye viwanja vikubwa jijini Madrid .
           
       

   Kipindi soka linaanza kutambulika jijini Madrid na Hispania ,viwanja vilikuwa ndani ya jiji la Madrid . Athletics Madrid I wakiwa wanategemea dimba la Athletic Club mnamo Mwaka 1905 walikutana katika uwanja Wa HIPODROMO uwanja ambao ndiyo Madrid walikuwa wakiutumia wakati huo.

  Baada ya hapo wakaenda kucheza viwanja vya Fuente Del Berro na Campo Del Retiro uwanja Wa kwanza Wa nyumbani wa Rojblancos (Athletico).

   Halafu uwanja Wa Estadio O'Dennel ukawa unatumika Kwa mechi zote za nyumbani /ugenini Kwa timu zote kama ambavyo Millan na Inter wanavyoutumia uwanja Wa  Stadiou Giussepe Meazza.

   

   Dimba la Verodlomo Ciudad Lienal lilitumika kwa ajili ya Derby mwaka 1923 kabla ya Estadio Chemartin baada ya hapo uwanja Wa mwanzo kabisa wa Estadio Metropolitano .

  Vita vilikuaja kuharibu uwanja huo wa Athletico na ikawabidi waende kuhamia kwanza Campo Ve dellecas na baadae  Chamartine.

    Mpaka kufikia katikati mwa karne iliyopita timu zote zikapata viongozi /Marais ambao walikuja kufanya mapinduzi makubwa na kuzipatia mwanga timu hizo . Hapo ndipo Santiago Bernabue  na Vicente Kaderone vikajengwa na kuanza kutumika na vilabu hivyo.

   Derby ya Madrid ndiyo mchezo ambao umejirudia sana katika historia ya soka nchini humo na umekuwa ukivuka mpaka mipaka ya nchi hiyo na kuchezewa nje ya nchi.

   Katika michuano ya ulaya Mwaka 1959, uwanja wa La Romareda ulitumika katika mchezo wa nusu fainali wa Madrid Derby .
Lisbon ukafatia Mwaka 2014 katika fainal I na Mwaka 2016 mtanange huo ukapigwa tena Giussepe Meazza.

  Leo tena wanakutana katika mchezo wa ligi kuu Spain Mmarufu kama La Liga huku Athletico akiwa hajapoteza hata mchezo mmoja na Real Madrid akiwa kapoteza michezo miwili . Athletico wapo katika nafasi ya tatu na Real Madrid wapo katika nafasi ya nne huku ligi hiyo ikitarajiwa kubadilika katika msimamo huo baada michezo ya usiku wa leo kumalizika .

                         Kwa mawasiliano :
                   Samwelim418@gmail.com
                               0625954293.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI NA MCHE YANARNDELEA .

BEBI MADAHA NA ISABELA WAHUSISHWA NA KUSAGANA

YANGA KUJA NA JEZI HIZI MSIMU 2017/2018.