DODOMA YACHEZEA KICHAPO NA JKT YANUSA LIGI KUU MSIMU UJAO.
Wakati mambo yakimwendela mlama Kocha Jamhuri Kihwelo "JULIO" timu ya JKT TAanzani imetanguliza muu mmoja ligi kuu ya VPL katika msimu ujao baada ya kuifumua timu MVUVUMWAFC kwa mabao 3-0 katika mfululizo wa mechi za ligi daraja la kwanza (FDL).
JKT ilipata ushindi huo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kufikisha point 28 ikisaliwa na michezo tatu kabla ya kumaliza msimu . Huku sasa ikihitaji point nne tu kupanda ligi kuu ya VPL msimu ujao
Ushindi huo umeifanya timu hiyo inayonolewa na kocha Bakari Shime kukaa kileleni mwa msimamo ikizidi kuziacha Friend Rengers na African Lyon zilizoko nyuma yake zikiwa na point 19 na 18 amabpo leo zitapetana katika mchezo mwingine wa ligi hiyo.
Kwa kuangalia uwiano wa point na Mabao tunawez kusema kuwa JKT wameshapanda ligi kuu na wanasubiria tu ratiba kuwaidhjnisha mwishoni wa ligi yao inagwa kwenye soka lolote linaweza kutokea .
Katika matokeo mengine ya ligi hiyo Dodona Fc imekutana na kichapo cha mabao 2 -0 ikiwa ugenini ambako imekubali kipigo kutoka kwa Rihno Rangers na kutibuliwa kasi yao ya kupanda ligi kuu hali ambayo imeikumba pia Alliance iliyokubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Biashara United mkoani Mara.
Bishara United imeishusha Dodoma Fc kileleni baada ya kufikisha Point 23 kwa 21 za Dodoma Fc vijana wa Julio huku Alliance ikisalia nafasi ya 3 katika kundi hilo la C wakiwa na alama zao 18.
Mjini Mbeya Mbeya Kwanza wametoka suluhu na KMC huku Mlale JKT ikishinda bao 1 - 0dhidi ya Mawenzi Market huku Costal Union ikishinda kwa magoli 3 - 0dhidi ya Mudindi United huku Kiluvya akipigwa bao 3 - 0 dhidi ya Mgambo JKT wakati huohuo Toto Africans ikilazimishwa sare na KJT Olijoro.
Imeandaliwa na Misangle .
Cont: 0625954293/0659116814
Comments